Tuesday, 9 August 2016


ARUSHA TAJIRI WA TANZANITE DUNIANI KOTE



Tanzanite ni madini yenye mchanganyiko wa rangi ya bluu na zambarau. Madini haya ni ya kipekee kwa Tanzania kwani hayana chanzo chochote duniani isispokuwa kile cha Mererani mjini Arusha, Tanzania.


Madini haya yaligundulika mwaka 1967 lakini yakajipatia jina hilo mwaka 1969 kutoka kwa Henry Platt, makamu wa rais katika kampuni ya Tiffany and Co. Juhudi za kutafuta soko la madini haya lilipa jina la Tanzanite umaarufu ndani ya mda mfupi hadi kutumika katika soko la madini kidunia. 

Kinachovutia zaidi kwenye madini haya ni uzuri wa rangi yake. Yapo madini haya yenye rangi ya bluu hadi yalio na rangi ya zambarau. Rangi yake hubadilika badilika kadiri unavyolitazama kupitia pembe tofauti.

No comments:

Post a Comment