Tuesday, 9 August 2016


ARUSHA MJI WENYE FURSA NYINGI


Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani ni kufuatana na mwendo wa saa: KilimanjaroManyaraShinyanga na Mara. Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa pili kwa Utajiri nchini Tanzania.
Wilaya zake ni MonduliLongidoMeruArusha VijijiniArusha Mjini,Ngorongoro na Karatu. Makao makuu yapo Arusha mjini.
 Milima yake Oldoinyo Lengai (2,878 m) bado nivolkeno hai, na mlima Meru ni volkeno ya kulala tangu mw. 1910. Mvua hunyesha kati ya millimita 1,800 mm kwa mwaka mlimani Arusha hadi 508 mm kwa mwaka katika maeneo makavu.
Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Barabara ya lami Dar Es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori NgorongoroSerengetiOlduvai, Arusha, Tarangire na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimajaro iko karibu.
Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti. fosphoras inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
Kati ya wakazi wa mkoa kiasili ni WaarushaWameruWairaqw na Wamassai.

No comments:

Post a Comment