Wednesday, 10 August 2016

MLIMA MERU


Ni mlima wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania ukiwa na kilele chenye urefu wa futi 14,980, kutoka usawa wa bahari nyuma ya mlima wa kilimanjaro.

Mlima Meru wenye muonekano mzuri ukiwa kati kati ya mji wa ARUSHA, ni moja kati ya milima ipatikanayo kaskazini mwa TANZANIA katika moyo wa hifadhi ya taifa ya Arusha.

Unaweza kupata muonekano bora na mzuri wa mlima kilima NJARO, ukiwa katika mlima MERU, kwani ni maili 50 kutoka mlima mmoja kwenda mlima mwingine. Mlima Meru ni chaguo muhimu kwa wale wanaotaka kuchanganya kupanda mlima huku wakishuhudia wanyama pori wakati wakikwea kilele cha mlima.

Unaweza kuona wanyama kama nyati, twiga, nyani, tembo pamoja na fisi kwa uchache, lakini inawezekana kuona hata chui japo sio kwa urahisi.

Utalii unaofanyika hapa ni utalii wa kupanda mlima, ekolojia na wa kuvinjari nyikani.

No comments:

Post a Comment