Friday, 26 August 2016

MAPIGANO POLICE NA MAJAMBAZI


Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

Wananchi walio eneo la tukio wameshuhudia magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru zimefungwa kutokana na mapambano hayo.

Inadaiwa wamekamatwa majambazi 14 na wengi wao ni askari wastaafu. Kiongozi wa wahalifu wao ni Kanali wa Jeshi mstaafu

No comments:

Post a Comment